Huduma Zetu

Usajili wa Hati

Usajili wa Hati

1.1 Utangulizi

Ofisi ya Usajili wa Hati inatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura Namba 334 (The Land Registration Act, Cap.334). Sheria ya Usajili wa Nyaraka Sura Namba 117 (The Registration of Documents Act, Cap.117), Sheria ya Usajili wa Mali zinazohamishika Sura Namba 210 (The Chattels Transfer Act, Cap. 210), Sheria ya umiliki wa sehemu ya Jengo (Unit Title Act No 17/2008).

Katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu hayo ofisi ya Usajili wa Hati ipo katika kanda nane za usajili katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Moshi, Mtwara, Mbeya, Tabora, Dar es Salaam na Morogoro.

2.1 Majukumu

Kusajili Hati na Nyaraka kulingana na sheria husika kama ifuatavyo;-

2.1.1 Chini Ya Sheria Ya Usajiliwa Hati Sura Na.334

(i) Hati za kumiliki ardhi (Certificate of Title);

(ii) Milki zilizouzwa (transfers);

(iii) Mikataba ya upangishaji;

(iv) Miliki zilizowekwa rehani (Mortgages) ;

(v) Rehani zilizomaliza deni (Discharge and Releases) ;

(vi) Nyaraka za kuwekesha Hati (Notice of Deposit);

(vii) Nyaraka za kuwekesha Hati zilizoondolewa (Withdrawal of Notice of Deposit);

(viii) Hati za marejesho ya miliki na miliki zilizofutwa (Surrender and Revocation);

(ix) Hati nyinginezo:-

o Maombi ya kuandikishwa wasimamizi wa Mirathi;

o Maombi ya kuandikishwa warithi wa marehemu;

o Mabadiliko ya majina ya wamiliki wa Hati za Kampuni au mashirika mbalimbali;

o Marekebisho ya Hati zilizoandikishwa kwa makosa (Rectification).

(x) Uhamishaji wa miliki unaotokana na maamuzi ya Bunge au sheria mbalimbali (Transmission by Operation of Law).

(xi) Nyaraka za Tahadhari na Vizuizi (Caveats & Injuctions).

(xii) Kutoa taarifa za upekuzi wa Daftari la Hati (Search reports).

(xiii) Utwaaji wa Ardhi (Aquisition of right of occupancy)

(xiv) Maombi ya hati mpya ( replacing lost certificates and mutilated )

(xv) Kusajili renewal of right of occupancy

(xvi) Application by adverse possession

(xvii) Application by survivor of joint tenants

(xviii) Deeds of variation & charges

(xix) Kutoa ushahidi mahakamani na kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu kesi zinazohusu usajili wa Hati na nyaraka mbalimbali

(xx) Kusajili Partition/Division of parcels

2.1.2 Chini ya Sheria ya Usajili wa Nyaraka (Sura 117)

(a) Nyaraka ambazo ni lazima zisajiliwe (Compulsory Registration

Uhamisho/mauzo ya nyumba/mashamba ambayo yana barua ya toleo;

o Mikataba ya upangishaji;

o Rehani;

o Ufutaji wa rehani zilizolipiwa;

o Barua za toleo zilizotolewa kwa maeneo ambayo hayajapimwa (Offer of Right of Occupancy) ;

o

(b) Nyaraka za Hiari (Optional Registration):

o Nyaraka zinazotoa mamlaka (Power of Attorney) ;

o Mabadiliko ya jina (Deed Poll) ;

o Nyaraka za uteuzi (Deed of Appointment) ;

o Nyaraka za maelewano (Memorandum of Understanding)

Wosia (Will);

o Mikataba ya Mauzo (Agreements for Sale);

o Barua za utoaji wa mali (Letter of Hypothecation of Goods)

o Hati ya dhamana (Indemnity Bonds) ;

o Mikataba ya kuingia ubia (Partnership Deeds) ;

o Mkataba wa kutoa huduma za kitaaluma ( Professional Service Contracts)

o Taarifa za upekuzi (Search Reports) na

o Nyaraka nyinginezo kama:

Ø Mikataba ya makabidhiano;

Ø Maombi ya kuvunja ubia;

Ø Viapo;

Ø Mikataba ya ukopeshaji;

Ø Makubaliano ya kuondoa madai;

Ø Mikataba ya kuwekesha Hati;

Ø Vizuizi;

Ø Mikataba ya ajira;

2.1.3 Chini ya Sheria ya Usajili wa Rehani za Mali Zinazohamishika (Chattels Transfer Act) Sura Na.210

Rehani zinazohamishika ambazo dhamana zake ni mali zinazohamishika kama magari, ndege, boti, pikipiki, vyomba vya nyumbani mashine za aina mbalimbali, samani na kadhalika. Rehani hizo husajiliwa katika kitengo cha usajili.

2.1.4 Chini ya Sheria ya Umiliki wa Sehemu ya Majengo (Unit Title Act Na. 17

Chini ya sheria hii miliki ya sehemu ya jengo au majengo husajili na kutolewa kwa mmiliki. Sheria hii imeweka masharti yanayopaswa kufuatwa na wamiliki wanaomiliki sehemu ya jengokwa ujumla wao. Pamoja na majukumu tajwa hapo juu kitengo kinahusika na kutunza hati na nyaraka zote zinazosajiliwa pamoja na kutoa taarifa za umkiliki pale inapohitajika.