Kurasa

MAJUKUMU

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayo majukumu yafuatayo:

 1. Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi;
 2. Kusimamia upangaji wa miji na vijiji;
 3. Kupima ardhi na kutayarisha ramani;
 4. Kutoa hati za kumiliki ardhi na hatimiliki za kimila;
 5. Kusajili hati za umiliki ardhi na nyaraka za kisheria;
 6. Kuthamini mali;
 7. Kuhamasisha na kuwezesha wananchi kuwa na nyumba bora;
 8. Kutatua migogoro ya ardhi na nyumba;
 9. Kusimamia upatikanaji na utunzaji wa kumbukumbu za ardhi;
 10. Kusimamia ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na huduma za sekta ya ardhi;
 11. Kusimamia Shirika la Nyumba la Taifa, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi na Wakala wa Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni;
 12. Kusimamia uendeshaji wa Vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro; na,
 13. Kusimamia maslahi na utendaji kazi wa watumishi wa sekta ya ardhi.