Serikali imewataka Wenyeviti wa Mbaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kujiepusha na tabia ya uwekaji mazuio yasiyo na tija dhidi ya uuzaji wa nyumba za wadaiwa wa benki.
Serikali ya Tanzania na Kenya zimekamilisha zoezi la uwekaji vigingi katika mpaka unaoigawa Tanzania na Nchi jirani ya Kenya katika mbuga ya Serengeti na hivyo kufanikiwa kumaliza mgogoro wa mpaka uliokuwepo hususani katika sekta ya utalii kati ya nchi zote mbili.
Serikali imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa kuhesabiwa katka sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Ageline Mabula amewataka wananchi kuipa kipaumbele sekta ya ardhi kwa kuwa sekta hiyo ikitumiwa vizuri itawezesha kuchochea mapinduzi kichumi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kufanikisha kuandaliwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi pamoja na upimaji ardhi kwenye vijiji vya Ntondo na Nkwea vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Singida katika mkoa wa Singida.
Wakati Serikali ya Awamu ya Sita kitimiza mwaka mmoja Machi 19, 2022 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameanika mafanikio ya serikali hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development