Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema Wizara yake haitarajii kuwepo makazi holela nchini baada ya mwaka mmoja kwa kuwa serikali ilijiwekea malengo ya miaka kumi ya kurasimisha maeneo ya makazi holela.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka waandishi wa habari nchini kutumia nafasi zao vizuri kuwa kama jicho la serikali katika kutoa elimu na ufahamu kwa wananchi kuhusu sekta ya ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema faida kubwa na kipaumbele katika zoezi la Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi ni kupambana na ukatili dhidi ya wanawake
Jumla ya vijiji 75 vilivyokuwa na migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa wa Arusha vimenufaika na hisani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kwake kubaki maeneo yake kufuatia vijiji hivyo kuingia kwenye migogoro ya matumizi ya ardhi na maeneo ya hifadhi.
Timu ya Wataalamu wa Mipaka kati ya Tanzania na Kenya imetembelea na kujionea kazi ya uimarishaji mipaka wa Kimataifa wa nchi hizo iliyofanywa kwa lengo la kukagua na kushauri namna bora ya kuendelea na kazi zinazofuta.
Waziri wa ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa onyo kwa wananchi wanaotumia hisani ya Rais Samia Suluhu Hassan kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyomegwa
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development