Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi leo amekutana na vyombo vya habari Nchini kutoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika Jengo la Wizara ya Ardhi Magogoni ifikapo tarehe 1, Agosti wafike ili waweze kutatuliwa kero na malalamiko ya ardhi yanayowakabili.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula anahudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa Victoria Falls Magharibi mwa Zimbabwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia kusamehewa riba ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu kwa masharti kwamba wadaiwa hao wawe wamelipa madeni yq msingi ndani ya miezi sita kuanzia mwezi julai hadi desemba 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi amewataka wataalamu wa utahamini kujitathmini katika kazi wanazozifanya ili kuepuka kufanya kazi kwa matakwa ya wale wanaowafanyia kazi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kutoa kipaumbele katika utengaji bajeti za ndani ili kuhakikisha mipango ya matumizi ya ardhi inaandaliwa katika vijiji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekabidhi Scanner 50 zenye thamani ya shilingi milioni 880 kwa kwa ajili ya kurahisisha zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali.
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development