Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Phillip Mpango amewataka viongozi wa dini nchini kuwafundisha na kulea vijana katika maadili mema pamoja na kuthamini kufanya kazi kihalali.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa wito kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kuweka mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo la Mradi wa wa Chanzo na Kituo cha Tiba ya Maji cha Butimba mkoani Mwanza.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amemshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha wizara yake kupata fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Viongozi wa Wilaya ya Handeni na Mkoa wa Tanga kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi katika maeneo yao ili kuepuka migogoro ya ardhi isiyo ya lazima baina ya wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabuka amewataka wananchi wote wanaonunua ardhi kufanya uhakiki kabla ya kununua kupitia ofisi za Halmashauri sambamba na kufanya Search kwa maeneo yaliyo na hati.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa onyo kwa viongozi wa vijiji na vitongoji kuacha mara moja kujivika madaraka na kuvunja sheria za ardhi kugawa ardhi kinyume na sheria na kusababisha uvamizi kwenye maeneo yenye milki za watu wengine.
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development