Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Kanda ya kati (Dodoma) yakusanya kiasi cha Tshs. 1,426,273,033.70 ya Makusanyo ya Kodi ya Pango la Ardhi, sawa na 204% ya malengo na hivyo kuvuka malengo iliyopangiwa
Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya nyanda za juu Kusini imekusanya jumla ya Tsh. 5.8 bilioni kodi ya pango la ardhi kwa kipindi cha kuanzi Julai 2016 hadi mei 2017 ikishirikiana na Halmashauri 34 zilizopo katika Kanda