Matawi 228 ya Benki ya NMB nchini katika kila eneo kupitia Mawakala wake zaidi 17,000 watasaidia kutoa huduma za ukadiriaji na kusanyaji kodi na tozo mbalimbali za ardhi nchini .
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameonya wale wanaoomba vibali vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati majengo
Serikali imeamuru vijiji vitano na vitongoji 47 katika vijiji 14 pamoja na sehemu ndogo ya kitongoji cha magwalisi kilichopo mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa wilaya ya mbarali kuhamishwa ili kupisha hifadhi.
Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia wananchi wa kitongoji cha Ikanka kijiji cha Itumba wilaya ya Ileje kuendelea kuishi sehemu ya eneo la hifadhi ya msitu wa Ileje Range mkoani Songwe
Serikali imeruhusu vijiji 46 katika mkoa wa Simiyu vilivyokuwa katika mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi kuendelea na shughuli za kibinadamu ambazo hazitaathiri shughuli za uhifadhi wa wanyama pori na ndani ya eneo kinga la mita 500.
Halmashauri ya Mji wa Newala mkoa wa Mtwara imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapima na kumilikishwa maeneo yake yakiwemo ya shule, zahanani na vituo vya mabasi ili kuepuka migogoro ya ardhi.
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development