Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanapokwenda kutatua migogoro ya ardhi wanakuwa na ufumbuzi badala ya kuwa chanzo cha migogoro.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametembelea eneo la Karikaoo kwa lengo la kuangalia namna bora ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga kutumia majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufanyia biashara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Wataalam wa Mipangomiji nchini kuhakikisha wanapopanga mipango yao kwenye maeneo mbalimbali nchini wanatenga maeneo ya wafanyabiashara wa kawaida ili waweze kufanya biashara katika mazingira rafiki na yaliyo bora.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewajia juu watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amefanya ziara ya kushtukiza ofisi ya ardhi ya halmashauri ya jiji la Dodoma na kuagiza maombi 521 ya umilikishaji ardhi katika ofisi hiyo kukamilishwa ndani ya siku tatu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde amesema kuanzia sasa ofisi yake haitasajili vijiji bila kushirikisha wadau muhimu ili kuondokana na migogoro ya matumizi ya ardhi inayojitokeza
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development