Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametaka elimu ya kuwatahadharisha wananchi kuhusu kujiepusha na vishawishi visivyo na tija vinavyosababisha ugawaji maeneo ya ardhi kwa ajili ya uwekezaj kwa kupewa ahadi zisizotekelezeka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia vijiji 67 vilivyokuwemo maeneo ya hifadhi katika mkoa wa Morogoro kubaki ili kuwawezesha wananchi wake kuendelea na shughuli zao bila matatizo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaonya wananchi wanaojenga au kupanda mazao kwenye maeneo yanayopangwa kutwaliwa na Serikali
Serikali imewataka Wenyeviti wa Mbaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kujiepusha na tabia ya uwekaji mazuio yasiyo na tija dhidi ya uuzaji wa nyumba za wadaiwa wa benki.
Serikali ya Tanzania na Kenya zimekamilisha zoezi la uwekaji vigingi katika mpaka unaoigawa Tanzania na Nchi jirani ya Kenya katika mbuga ya Serengeti na hivyo kufanikiwa kumaliza mgogoro wa mpaka uliokuwepo hususani katika sekta ya utalii kati ya nchi zote mbili.
Serikali imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa kuhesabiwa katka sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development