Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemkabidhi Ofisi aliyekuwa Naibu wake Dkt Angeline Mabula ambaye sasa ni Waziri wa Wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuendelea na ujenzi wa miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa iliyosimama.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wizara yake itaanza ukaguzi na kuyatambua maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji nchini.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekamilisha uandaaji ramani za kidijitali zinatotumika kama ramani za msingi kwenye utekelezaji mfumo wa anuani za makazi katika halmashauri 38 nchini.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa siku 60 kuanzia tarehe 5 Februari 2022 kuhakikisha wamiliki wa ardhi waliopimiwa viwanja kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi huku wale wenye miliki za ardhi wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi.
Katika kuhakikisha mlundikano wa mashauri ya migogoro ya ardhi unapungua nchini, Msajili wa Mabaraza ya Ardhi Stela Tullo ameelekeza Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwenda kusikiliza mashauri katika wilaya nyingine ambazo hazina wenyeviti.
© 2023 All Rights Reserved.
Site Map
Staff Mail
Designed and Developed bylbl_ega_nam (e-GA) and Contents Managed by Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development