KAMPENI YA UHAMASISHAJI ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI
Posted On: 17th August, 2016
WIZARA YA ARDHI KATIKA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WA KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI
NA UTOAJI WA ELIMU YA SEKTA YA ARDHI
Serikali
ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Rais John pombe Magufuli imetangaza mabadiliko
makubwa yanayolenga kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kodi mbalimbali
kwa maendeleo ya Taifa letu.
Kutokana na azma hiyo, Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inalo jukumu la kukusanya kodi ya pango la
ardhi ambayo inatozwa kwa wamiliki wa viwanja na mashamba yaliyopimwa
na kumilikishwa kisheria.
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini kwa kushirikiana na Kitengo cha kodi katika Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kimefanya kampeni maalumu ya
uhamasishaji wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi na utoaji wa elimu ya sekta
ya ardhi.
Kampeni
hii ilifanywa jijini Dar es salaam katika Manispaa za Ilala, Kinondoni na
Temeke ambapo wananchi walifikiwa moja kwa moja na kupewa vipeperushi na stika
za kubandika katika magari, Bajaji na vyombo vingine vya moto na hata katika
nyumba na maduka.
Elimu
ilitolewa kwa wananchi kuhusu ulipaji wa kodi ya Pango la Ardhi ambayo hulipwa
katika halmashauri zote nchini na katika kituo cha makusanyo cha Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wananchi
katika maeneo ya Temeke wakihamasika kuchukua vipeperushi mbalimbali vya
wizara, wakati wa Kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi.
Ndani ya gari ni kikundi cha Fataki,
ambacho kimeshiriki katika kutoa elimu hiyo kwa njia ya mashairi. Uhamasishaji
huo umefanyika katika wilaya tatu za Dar es Salaam (Ilala, Temeke na
Kinondoni).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo
ya Makazi, Mboza Lwandiko akiwagawia vipeperushi wakazi wa Mbagala, katika uwanja
wa Zakhem, wakati wa Kampeni ya uhamasishaji wa kulipa kodi ya pango la ardhi.
Uhamasishaji huo umefanyika katika wilaya tatu za Dar es Salaam ( Ilala, Temeke
na Kinondoni).
Afisa Habari wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Rehema
Isango akiwagawia vipeperushi wakazi wa Mbagala, wakati wa Kampeni ya
uhamasishaji wa kulipa kodi ya pango la
ardhi. Uhamasishaji huo umefanyika katika wilaya
tatu za Dar es Salaam (Ilala, Temeke na Kinondoni).
Rahma Moyo, kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Ardhi akibandika stika yenye
ujumbe wa kuhamashisha ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi, kwenye gari la mmoja
wa wakazi wa Dar es Salaam, wakati wa Kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji wa
kodi ya pango la Ardhi.