KOREA YASHIRIKIANA NA WIZARA YA ARDHI KUBORESHA UPIMAJI NCHINI
Posted On: 10th June, 2016
Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata
vifaa vya upimaji (Total Station) na kutegemea kupata mafunzo kuhusu
matumizi yake kuanzia tarehe 13 Juni – 16 juni, 2016 kutoka nchini Korea.
Akikaribisha ujumbe
wa Wakorea hao Wizarani, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bwn. Justo Lyamuya
amesema kuwa vifaa hivyo vya upimaji vitasaidia kuhuisha ramani zilizopitwa na
wakati.
Bwn. Lyamuya ameelaza
kuwa, idadi ya vifaa vya upimaji vitakavyotolewa wakati wa mafunzo, vitakuwa vinne
(4), (Total Stations).
Kwa upande wake
Munseok Lee, kiongozi wa ujumbe huo, alitoa ufafanuzi kwa vitendo kwa kifupi
kuhusu matumizi ya kifaa cha upigaji picha za anga, kwa ndege, isiyokuwa na
Rubani (drone) na kuahidi kutoa ufafanuzi wa kina zaidi kwa siku 4 (tarehe 13 –
16 juni), wakati wa mafunzo yatakayofanyika kwa Maafisa waliopo kwenye kada ya
Upimaji na Ramani.
Vifaa hivyo
vimetolewa na nchi ya Korea kwa nia ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania
na Korea.