WIZARA YA ARDHI YATOA SIKU 60 WENYE VIWANJA VILIVYOPIMWA KUWASILISHA MAOMBI YA KUMILIKISHWA
Posted On: 04th February, 2022
Na Munir Shemweta, WANMM
Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa siku 60 kuanzia tarehe 5
Februari 2022 kuhakikisha wamiliki wa ardhi waliopimiwa viwanja
kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi huku wale wenye miliki za ardhi
wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari leo tarehe 4 Februari 2022, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na ,Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi
alisema, mmiliki ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa, Serikali
itachukua hatua za kisheria ikiwemo kufuta miliki, kupiga mnada na
kumilikisha viwanja vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.
‘’Mmiliki
ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa Serikali itachukua hatua
za kisheria ikiwemo kufuta miliki, kupiga mnada na kumilikisha viwanja
kwa wananchi wenye uhitaji, hatua hizi zitaanza kuchukuliwa tarehe 6
April 2022’’ alisema Dkt Kijazi .
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ni
wajibu wa kisheria kwa wamiliki amabao ardhi zao zimepangwa na kupimwa
kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi kwa Kamishna wa Ardhi ili
kumilikishwa sambamba na kulipa kodi ya pango la ardjhi.
‘’Ni
wajibu wa kisheria kwa wale wamiliki wa ardhi ambao ardhi zao
zimepangwa na kupimwa kuwasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi kwa
Kamishna wa Ardhi kwa ajili ya kumilikishwa na kulipa kodi ya pango la
ardhi’’ alisema Dkt Kijazi.